Logo

Bitcoin Circular Communities

NOV20
Friday, November 20, 202608:00 PM - 09:30 PM
location_on
Tanzania
About Event

Habari Mtanzania! GOOD NEWS! DARASA LA KIJAMII ZAIDI! ๐ŸŒโ™ป๏ธ

Umeshawahi kujiuliza inawezekanaje kijiji kizima kikatumia Bitcoin kama pesa ya kila siku? Kama Shilingi?

Ndugu yangu, kama ndoto hiyo imewahi kupita kichwani mwako, basi tambua kwamba tayari inatokea duniani, na sasa ni zamu yetu Tanzania!

Tarehe 20 Novemba 2026, tutakuwa LIVE kwenye Google Meet katika darasa la kipekee na la kuleta matumaini makubwa: "Bitcoin Circular Communities - Jumuiya Zinazotumia Bitcoin kwa Mzunguko."

Hii ndio hatua inayofuata na muhimu zaidi ya mapinduzi ya Bitcoin! Mapinduzi haya sio tu ya kununua Bitcoin na kuihifadhi (HODL) kwenye simu yako ukisubiri ipande bei. Hapana! Mapinduzi ya kweli ni pale tunapoanza kuitumia Bitcoin kama pesa halisi ya kila siku - kununua mahindi sokoni, kulipia bodaboda, kunywa kahawa, kulipia umeme na huduma zote za kijamii!

Darasa hili lenye maono makubwa litaongozwa na mwalimu wetu mwenye mapenzi na jamii, Mwalimu Graysatoshi , ambaye atatupeleka kwenye safari ya kimataifa ya kujifunza:

โœ… Nini maana halisi ya Bitcoin Circular Economy kwa lugha rahisi kabisa ambayo kila mtu anaweza kuelewa?
โœ… Mifano halisi inayofanya kazi duniani Tutajifunza kutoka kwa wahenga kama Bitcoin Beach ya El Salvador, Bitcoin Ekasi ya Afrika Kusini, na Bitcoin Witsand na jinsi walivyofanikisha.
โœ… Jinsi ya kuanzisha jumuiya ya Bitcoin mtaani kwako - Hatua kwa hatua, kuanzia na marafiki zako watatu.
โœ… Faida kubwa kwa wafanyabiashara wadogo kukubali Bitcoin kama malipo na jinsi inavyowavutia wateja wapya.
โœ… Na sisi kama familia ya BitcoinSafariTz tunawezaje kwa pamoja kujenga Tanzania ya kwanza ya Bitcoin?

Kama wewe ni kiongozi wa jamii, mjasiriamali, mama ntilie, au kijana mwenye maono ya kubadilisha mtaa wako, hili ndilo darasa lako muhimu la mwaka!

Usikose kujifunza jinsi tutakavyobadilisha Tanzania kwa kutumia Bitcoin!

Link ya Darasa Hapa ๐Ÿ‘‰ https://calendar.app.google/zFNCozkcZkPbXRMb8

Karibu sana, elimu ni bure na uhuru ni kwa wote!

Location
Tanzania